Ofisi ya utabiri wa hali ya hewa, imesema mvua nzito zina weza sababisha mafuriko katika maeneo ya Illawarra, Blue Mountains, maeneo ya jiji la Sydney na katika sehemu za kanda la Hunter na wilaya za Central Coast.
Kituo cha usimamizi wa usafiri kime shauri dhidi ya safari zisizo mhimu na, kimeonya kuhusu kuchelewa namapengo katika huduma za usafiri wa umma. Watu wameshauriwa wacheleweshe safari zozote zinazo husiana na likizo za shule pia, wakati amaeneo ya pwani ya kusini yakiwa katika hatari ya mafuriko ya muda mrefu.
Mawimbi yenye urefu wa mita tano, nayo yanaweza sababisha mmonyoko katika maeneo ya pwani.