Hatua ya Rais Kenyatta imechukuliwa kama ni njia ya kuwaadhibu majaji hao, kwa misimamo na maamuzi yao. Rais Kenyatta ameshtumiwa pia kwa kukiuka amri za mahakama mara kadhaa.
Mvutano waendelea kati ya ofisi ya rais na mahakama Kenya

Rais Kenyatta akiwa nama afisa wa mahakama nchini Kenya Source: State House Kenya
Rais Uhuru Kenyatta ameshtumiwa kwa kukiuka sheria baada ya kukataa kuwateua majaji sita kati ya arobaini, walio kuwa wamependekezwa na tume ya huduma ya mahakama.
Share