Vijana wa timu ya Jamhuri ya Congo walijua matokeo yoyote yasiyo ushindi yange maanisha mwisho wao katika kombe hilo. Licha yakupokea kadi mbili nyekundu katika mechi yao dhidi ya vijana wa Ghana, vijana wa Jamhuri ya Congo walitekeleza wajibu wao nakushinda mechi yao kama ilivyo takiwa.
SBS Swahili ilizungumza na Mwalimu wa timu hiyo Bw Benin pamoja na nahodha wake Bw Akram, ambao waliweka wazi walivyu kabili changamoto yakufuzu kwa robo fainali. Wawili hao walifunguka pia kuhusu kombe la dunia litakalo anza katika siku chache nchini Qatar, pamoja na matarajio kwa timu wanazo shabikia.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.