Tangazo hilo lime jiri siku chache baada ya kutolewa kwa ripoti ya tume ya uchunguzi kwama benki, ambamo wawili hao walipokea ukosoaji maalum.
Ripoti hiyo ilitoa hukumu katika sekta hiyo iliyo ongozwa kwa tamaa, pamoja nakutoa mapendekezo 76 yakutoa ulinzi bora kwa wateja pamoja naku boresha udhibiti. Ripoti hiyo ili gusia pia visa 24 vya uwezekano wa uhalifu, kwa wasimamizi wahusika wafanyie uchunguzi wa ziada.
Baada ya matangazo ya viongozi hao kujiuzulu, je hatua za ziada zakisheria zitachukuliwa dhidi yawalio kosolewa vikali kwaku shiriki katika matendo yanayo dhaniwa kuwa niya kihalifu?