Shirika la Nakango Vision lina andaa tamasha ya vyakula vya tamaduni tofauti, Jumamosi 10 Novemba 2018. Shirika hilo lita toa mafunzo pia kupitia washiriki wao kuhusu haki za binadam katika tamasha hiyo.
SBS Swahili ilizungumza na mchungaji Nava Ozegbe ambaye ndiye mwanzilishi wa shirika la Nakango Vision kuhusu tukio hilo.
Tamasha hiyo ita anza saa tisa mchana hadi saa kumi na mbili jioni, anwani ya sehemu ambako tamasha hiyo ita andaliwa ni 25 Barbara Street, Fairfield, NSW, Australia.
Share






