Hata hivyo, kuna baadhi ambao wamepiga kura zoa mapema tayari, na wagombea wa vyama vikuu kwa wagombea huru wame kuwa wakipiga doria nje ya vituo vyakupigia kura, kujaribu kuwashawishi wapiga kura katika sekunde za mwisho kabla wafanye maamuzi yao.
Mchungaji Navazu Ozegbe ni mgombea huru wa udiwani katika halmashauri ya jiji la Fairfield, New South Wales. Alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS nje ya kituo kimoja chakupigia kura, kilicho mshawishi kuwania nafasi hiyo, pamoja na sera anazo wauzia wapiga kura.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.