Wakati huo huo ni moja ya sehemu ngumu pia kupata nyumba ya kukodi.
Wiki hii tuta tazama aina ya makaazi yanayo hudumia kwa kipekee mahitaji ya wanafunzi.
Msako wa makaazi unastahili anza punde unapo thibitisha ambako utasomea. Utahitaji makaazi yanayo ambatana na bajeti yako, sehemu unako taka ishi pamoja na aina ya maisha yako.
Mbali na chaguzi za makaazi ndani ya vyuo, baadhi ya vyuo pia huwa na hifadhi data zao za makaazi ya nje ya chuo.
Hifadhi data hizi zinaweza tumiwa na wanafunzi wote wa sasa na wanafunzi watarajiwa, na hutoa rasilimali mhimu kwa kupata chaguzi mbadala za makaazi ambayo yako nje ya vyuo.