Kabla ya kongamano hilo, shirika la habari la SBS lilizungumza na wataalam wanne, watetezi na wahanga kuhusu kinacho stahili toka kwenye kongamano hilo.
Wakati mpango wakwanza wakitaifa wakupunguza unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wao ulipo undwa katika mwaka wa 2010, mwanamke mmoja katika wanawake watatu nchini Australia walikuwa wame pitia uzoefu wa unyanyasaji wakimwili tangu wakiwa na miaka 15, wakati karibu mwanamke mmoja kati ya wanawake tano, walikuwa wamepitia uzoefu wa unyanyasaji wa ngono.
Wasikilizaji wanao hitaji taarifa kuhusu unyanyasaji wakifamilia na ngono, au msaada wanaweza piga simu kwa namba hii: 1-800 RESPECT namba hiyo kwa ukamilifu ni 1800 737 732 na tovuti yao ni www.1800respect.org.au