Imani hiyo ilijengwa pia na jinsi serikali hiyo ilivyo simamia janga la Coronavirus, na kwa sababu hakuna serikali yoyote nchini iliyokuwa ime shindwa katika uchaguzi katika wakati huu wa janga.
Hata hivyo upinzani ulikuwa na maoni na sera tofauti ambazo, iliwauzia wapiga kura hadi dakika ya mwisho ya kampeni na matunda yake yalivunwa masaa machache baada ya vituo vya kura kufungwa kote jimboni.
Stephen Tongun ni makaaji na mwanasheria mjini Adelaide, Kusini Australia. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS aliweka wazi baadhi ya maswala ambayo wapiga kura wengi walizingatia kabla yakupiga kura zao. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.