Ilikuwa usiku wenye baridi sana tarehe 29 Agosti 2017, SBS Swahili ilipowasili katika eneo la Newtown Square katika kitongoji cha Newtown NSW.
Shirika la Newtown Neighbourhood Centre, lilikuwa lime andaa tukio ambapo watu walijitolea kulala nje kwa ajili yaku ongeza uelewa wa maswala ya wanao lala nje kwa sababu ya uhaba wa nyumba, au hawa wezi mudu gharama zaku kodi nyumba.

SBS Swahili ilizungumza na Catherine ambaye alikuwa amejitolea kushiriki katika mradi huo waku ongeza uelewa wa masaibu ya wanao jikuta katika mazingira yanayo wafanya wakose sehemu zaku ishi na uhaba wa nyumba za bei nafuu.
Share





