Nadia Murad na Dkt Denis Mukwege walipokea tuzo hizo katika sherehe iliyo andaliwa nchini Sweden ila, wawili hao wamesema kazi yao ya uanaharakati bado ita endelea.
Uamuzi waku mulika kampeni dhidi ya unyanyasaji wakingono, ulijiri baada ya tuzo ya maandishi ya nobel kuahirishwa kwa sababu ya kashfa ya ubakaji. Jean-Claude Arnault mwenye umri wa miaka 72, ni mume wa mwanachama wa bodi ya academy ya Sweden, alipatwa na hatia mapema mwezi huu (3 disemba 2018) wa mashtaka mawili ya ubakaji.
Alipewa hukumu ya miaka mbili na nusu gerezani kwa uhalifu huo na, wanachama wanane wa bodi hiyo wame jiuzulu au kujitenga na bodi hiyo kwa sababu ya kashfa hiyo.