Watu wengi wanao wasili nchini kama wakimbizi kawaida huja wakiwa katika familia zenye watu wengi.
Hali hiyo humaanisha wengi wao, hukabiliana na changamoto kubwa yakupata makazi yanayo tosheleza mahitaji yao, na wengi wao hukabiliwa na pigo baada ya lingine kutoka mawakala wa nyumba ambao hukataa maombi yao ya nyumba zinazo kidhi mahitaji ya familia zao.
Makala haya yanachunguza mchakato wakupata nyumba zinazo kidhi mahitaji ya familia, hususan familia zenye watu wengi ambao wanaishi katika nyumba ambako wanabanana kwa sababu ya uhaba wa nafasi.