Wachambuzi wamesema waendesha magari wa Australia watalipa zaidi katika vituo vya mafuta, katika siku zijazo na wameonya kuwa, hiyo ni ongezeko ya bei ambayo itaendelea kuongezeka kwa muda mrefu.
Australia ina petroli na mafuta ambayo hayaja safishwa kutumiwa nchini kwa muda wa siku 28, ambayo ni kidogo kama inavyo takiwa katika makubaliano yakimataifa, ambayo yanahitaji nchi kuwa na mafuta yakutosha kutumiwa kwa muda wa siku 90.
Mwezi jana Angus Taylor ali thibitisha kuwa Australia inafanya mazungumzo na marekani, kutumia petroli yake iliyo hifadhiwa.
Wakati huo huo chama cha Labor kimesema kuwa hiyo sio suluhu fanisi kwa usalama wa mafuta, kwa sababu haitapiga jeki usambazaji wa mafuta nchini.
Mbunge huru Andrew Wilkie amesema ni udanganyifu kuwasilisha mpango kama suluhu, wakati unategemea sana wema na hautoi maelezo kuhusu uhaba kimataifa.