Taifa hilo liko katika hali ya mshtuko baada ya watu kadhaa kuuawa na wengine kujeruhiwa, baada ya mshambuliaji kumimina risasi kadhaa ndani ya misikiti miwili katika eneo la kusini la mji huo.
Polisi wame sema wame wakamata watu wanne tayari, watatu ni wanaume na mwanamke mmoja ambao wako mbaroni sasa, pamoja naku weka magari kadhaa yaliyo kuwa na vilipuzi chini ya udhibiti wao.
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison, amethibitisha kuwa mmoja wa wanaume ambao wame wekwa kizuizini ni raia wa Australia, pamoja nakusema kuwa mwanaume huyo ni "gaidi wa mrengo wakulia".
Shirikisho la halmashauri zaki Islamu za Australia, lime toa mawazo na maombi kwa waathiriwa, wahanga, familia zao pamoja na watu wa New Zealand.
Dr Rateb Jneid ndiye rais wa shirika la Muslims Australia, amehamasisha misikiti yote pamoja na sehemu zote za ibada nchini Australia kuwa angalifu zaidi, nakwa wanachama wa jamii yawaislamu kuwa makini zaidi kuhusu usalama wao katika siku zijazo.