Baadhi ya vikundi kama wanawake wajawazito, wa Australia wa kwanza na watu wanao ishi katika vijiji nchini Australia hubeba mzigo mzito zaidi.
Zaidi ya idadi yawa Australia milioni 1.3, kwa sasa wanaishi na ugonjwa wa kisukari kwa maana ya mtu 1 katika watu 20 miongoni mwetu. Na takwimu hiyo inaendelea kuongezeka.
Kati ya mwaka wa 2000 na 2021, idadi ya watu walio kuwa waki ishi na ugonjwa wa kisukari ulikaribia kuongezeka mara tatu kutoka idadi ya watu 460,000 hadi watu milioni 1.3.
Katika mwezi wa Mei, serikali ilizindua uchunguzi bungeni kwa ugonjwa wakisukari, kwa ajili yaku elewa vizuri zaidi tatizo hili linalo ongezeka.
Shirika la National Rural Health Alliance linataka uwekezaji mwingi zaidi utolewe kwa uelewa, kutambua pamoja na miradi yakuzuia.
Mawasilisho kwa kamati hiyo ya uchunguzi kwa ugonjwa wakisukari kwa sasa yamefungwa, tarehe ya lini ripoti ya mwisho kwa uchunguzi hiyo ita tolewa, bado haija tangazwa.