Kuna wito kwa serikali ikate kodi ya mafuta, wiki mbili tu kabla ya bajeti ya shirikisho kutangazwa.
Kampuni ya Newspoll hufanya kura za maoni kwa maswala mbali mbali, imetoa vidokezo kwa maoni ya wapiga kura kuhusu uchaguzi mkuu ujao. Kura za kwanza cha chama cha Labor na za chama cha mseto hazija badilika. Katika kura za upendeleo kati ya vyama viwili, upinzani bado unaongoza kwa alama 10. Na kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka mbili, Anthony Albanese ana upendeleo sawia na Scott Morrison kama 'waziri mkuu bora' miongoni mwa wapiga kura.
Hata hivyo, matokeo ya kura halisi yatakuwa yale ya siku ya uchaguzi, ambao bado hauja tangazwa.