Matokeo ya utafiti huo yame jumuishwa katika ripoti ya kielezo cha gharama yakuishi, iliyo andaliwa na shirika la Anglicare Australia.
Ripoti hiyo imeonesha kuwa makaazi ni sehemu ya gharama kubwa ambayo wa Australia wenye mishahara ya chini wanakabili.
Alipo zungumzia hoja hiyo, waziri wa huduma zajamii, Amanda Rishworth, amesema bajeti ya shirikisho ya mei ilitoa malengo ya afueni kwa gharama ya maisha yenye thamani ya $14.6 bilioni, pamoja na nyongeza ya dola milioni 15.7 kwa uwekezeaji wa ufadhili wa mgogoro wa kiuchumi.