Kamishna wa masuala ya Ubaguzi wa rangi anayemaliza muda wake wa uongozi amesema, Australia inaonekana kutotilia mkazo suluhisho la kisiasa au viongozi kuwa na mazungumzo juu ya ubaguzi wa rangi.
Dr Tim Soutphommasane, alitoa maoni hayo wakati wa hotuba yake ya mwisho kama kamishna, akiwatuhumu wanasiasa na vyombo vya habari kutumia ubaguzi wa rangi kujipatia fedha au faida kisiasa.
Mwanasheria Mkuu wa Shirikisho Christian Porter, bado hajatangaza nani ata rithi wadhifa wa Dr Soutphommasane.
Share






