Wakristo kote nchini Australia wamejumuika makanisani kuadhimisha pasaka.
Jumapili ya pasaka huwakilisha siku ambayo wakristo wana amini Yesu kristo alifufuka kutoka wafu, baada yakusulubiwa siku ya ijumaa.
Wahubiri wakila dhehebu laki kristo, wame tumia siku ya leo kusambaza ujumbe wa matumaini.
Mchungaji David Runezerwa kutoka kanisa la Sing Hozana Outreach, alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS, umuhimu wa Pasaka kwake na waumini wa kanisa lake, pamoja na umuhimu wakusambaza ujumbe wa matumaini katika jamii na dunia.
Share






