Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Australia yanapo endelea kutangazwa, SBS Swahili ilizungumza na Bi Lucy Gichuhi, mgombea wa chama cha Family First ndani ya Seneti katika mkoa wa Kusini Australia. Bi Lucy alizungumzia mchakato wa kampeni pamoja na hatua yake yaku gombea kiti katika seneti.
Wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu, Waziri Mkuu wa Australia kwa ushirikiano na chama cha Australian Greens ali pitisha mswada bungeni ambao lengo lake lilikuwa kupunguza uwezekano wa wagombea huru na vyama vidogo kupata kura zakutosha kuingia bungeni.
Hatua hiyo ilichukuliwa kwa sababu ya matatizo ambayo serikali ilikuwa ikikabiliana nayo kutoka kwa baadhi ya wabunge huru na vyama vidogo ambavyo mara nyingi huwa havi pitishi miswada ya serikali.
Hata hivyo wapiga kura wame toa kura zao kwa wagombea huru na vyama vidogo, hatua ambayo itaendelea kuwa mwiba kwa Waziri Mkuu.
Share
