Maafisa wa ngazi za juu wamesema kuwa, wanawake wanaovaa hijabu wamekuwa wakitukanwa katika umma, baada ya shambulizi hilo lililofanywa na mwanaume aliyezaliwa Somalia. Idara hiyo ya Polisi imetupilia mbali pia, mapendekezo kuwa motisha ya mshambuliaji huyo, ilikuwa kile ambacho kimeripotiwa kuwa ni itikadi kali za kiislamu.
Watu wa Melbourne wametoa heshima zao za mwisho leo jumanne tarehe 20 Novemba 2018, kwa marehemu Sisto Malaspina ambaye alikuwa mmiliki wa mgahawa maarufu kwa jina la Pelligrini's.
Umma ulijumuika ndani ya kanisa la Saint Patricks, kumuaga marehemu Sisto, katika ibada iliyosimamiwa na serikali ya Victoria.