Wanasiasa hao wanatoka katika mirengo tofauti yaki siasa, na baadhi yao wali hudumu katika vikosi maalum, wengine walikuwa marubani na mmoja ni jenerali mstaafu.
Baadhi ya wanasiasa hao, wame changia maoni yao na shirika la habari la SBS, kuhusu maana ya Anzac Day kwao.
Bunge lime watambua wanasiasa wapatao 119, walio hudumu katika jeshi katika vita vya kwanza vya dunia. Hakuna mbunge wa shirikisho aliye fariki katika vita hivyo.
Huu ndio mwaka wa mwisho wa miaka mia ya Anzac.
Itakuwa ni miaka 100 tangu mwafaka waku sitisha vita kutiwa saini, na kutangazwa kwa mwisho wa vita.