Umaarufu wa tamasha hiyo umekuwa sana, kiasi kwamba zaidi ya watu elfu arobaini wame kuwa wakihudhuria tamasha hiyo kila mwaka.
Wanakamati wa tamasha hiyo Bi Poni na Katinda, wali eleza SBS Swahili kuwa wanatarajia kupokea zaidi ya watu elfu sitini mwaka huu.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya tamasha hiyo wapenzi wa muziki na tamaduni zawa Afrika watapata burudani kwa siku tatu kuanzia Ijumaa 18 Novemba, Jumamosi 19 Novemba na Jumapili 20 Novemba 2022 katika ukumbi wa Federation Square ambao uko katikati ya jiji la Melbourne.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili, pamoja na hapa chini kwa taarifa ya ziada kuhusu tamasha hiyo. www.africanmusicfestival.com.au