Walengwa zaidi wa mradi huo ni wanawake waliokosa elimu kutokana na mimba za utotoni, wajane pamoja na vijana waliomaliza masomo bila kupata ajira.
Popoli Frateli yatoa fursa mpya za ajira kwa vijana wa Kongo
Wanafunzi wa Popoli Frateli DR Congo Source: Byobe Malenga
Katika mpango wakuwataka vijana kubuni ajira wenyewe bila kutegemea kuajiriwa, shirika la POPOLI FRATELI katika mji wa Uvira ambao uko katika mkoa wa kivu ya kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imezindua kituo cha mafunzo kwa vijana ili kuwapa mafunzo ya kazi mbalimbali zikiwemo kazi za mikono.
Share




