Alipo hojiwa kuhusu mkutano huo, Prof Kitwaja kutoka chuo cha Arusha alionya kwamba "Afrika lazima ijipange vizuri ili inufaike kupitia uhusiano wake na Marekani".
Katika taarifa zingine kutoka bara la Afrika, bunge la Msumbiji limeidhinisha mswaada wa sheria inayohalalisha kujihusisha kwa wanamgambo katika vita dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado. Wanamgambo wa jimbo hilo wamekuwa wakisaidia jeshi na washirika wao kutoka Rwanda na Jumuia ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika katika vita dhidi ya wapiganaji wa kislamu katika jimbo hilo.
Na nchini Uganda, Rais Museveni, ameondoa vizuizi vyote vinavyohusiana na Ebola, akisema kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki imepiga hatua katika kukabiliana na ugonjwa huo hatari. Museveni amefuta vizuizi vyote vilivyowekwa katika wilaya ya Mubende, ambayo ndio ilikuwa kitovu cha ugonjwa huo, kulikoshuhudiwa visa 66 vya maambukizi na vifo 29, na katika eneo la Kassanda lililokuwa na visa 49 na vifo 21.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa zaidi kwa mwandishi wetu Jason Nyakundi.