Idara ya huduma za jamii katika serikali ya madola, imewekeza mradi huo nakushirikisha ma shirika yajamii zenye tamaduni mbali mbali kote nchini, kusimamaia mradi huo unao wapa fursa watu wenye ulemavu ndani ya jamii husika fursa yaku changia uzoefu wao wakuishi vizuri na ulemavu kupitia makala yaliyo rekodiwa.
Joy Rahab Sinclair ni afisa anaye husika kuwa andaa watu wanao ishi na ulemavu, kuchangia uzoefu wao pamoja nakuchapisha makala hayo. Alieleza idhaa ya Kiswahili ya SBS jinsi mradi huo unasaidia jamii zenye tamaduni mbali mbali kujua jinsi yakuishi vizuri na ulemavu. Kwa taarifa zaidi kuhusu mradi wa Speak My Language tembelea tovuti yao: www.speakmylanguage.com.au
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.