Jimboni Queensland Jamii yawatu kutoka kanda ya Afrika ya kati imekabiliwa kwa kesi zakusikitisha ambako, baadhi ya familia zimewapoteza wapendwa wao hali ambayo inge epukwa, kama kuna mtu katika familia husika aliyekuwa na ujuzi wakutoa huduma ya kwanza pamoja na ujuzi wakuzungumza Kiingereza.
Bw Luundo Rajabu alichukua hatua yakushughulikia swala hilo, kwakufungua shule kwa jina la Webster College ambako anafunza mbinu mbali mbali zakuokoa maisha. Katika mahojiano na SBS Swahili, Bw Rajabu aliweka wazi changamoto na mafanikio yakufungua shule hiyo, pamoja na mapokezi ya jamii kwa mafunzo anayo toa katika shule yake.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.