Hatakama taratibu nyingi za mafungo zina ambatana na mazoea ya msingi, baadhi ya taratibu hizo zina tofautiana kulingana na sehemu ambako mtu yuko.
Mafungo ya Ramadan ya mwaka huu, yamejiri miezi michache tu baada ya mashambulizi katika misikiti ya mji wa Christchurch, ambayo yamesababisha misikiti mingi nchini Australia kuongeza ulinzi wao.
Masaa ya Australia hufanya mafungo ya Ramadan kuwa rahisi, wengi wao mwaka huu watafanya mafungo, kwa muda wa masaa 12 kwa siku pekee.
Baadhi yawatu barani Ulaya watakuwa na jua kwa muda mrefu kidogo kila siku, kumaanisha itawabidi wafanye mafungo kwa muda wa masaa 19. Kuna wakati katika mwaka ambapo, katika sehemu chache ambazo ziko juu ya eneo la duru la arctic, ambako jua huwa halitui.
Katika visa kama hivyo, mamlaka wame toa mwongozo kuwa, waislamu wanaweza funga sawa na nchi ya kiislamu ambayo iko karibu yao, au sambamba na Mecca, Saudi Arabia ambako Uislamu ulizaliwa.