Jamii yawa Afrika jimboni New South Wales inasherehekea kutambuliwa kwa mchango wa balozi wao Rosemary Kariuki, katika tuzo za New South Wales Australian of the Year.
Bi Rosemary amekuwa akitetea maslahi yawanawake na wa Afrika kwa ujumla jimboni New South Wales kwa miaka mingi, kupitia miradi mbali mbali ambayo imeleta mabadiliko mengi chanya katika jamii nyingi.
Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bi Rosemary alitueleza alivyo jihisi kupendekezwa katika kamati inayo toa tuzo hiyo, harakati anazo fanya zakutetea jamii, na jinsi atakavyo kabiliana na jukumu lakuwa mshindi wa tuzo ya shujaa wa jamii jimboni New South Wales, hadi mshindi mwingine atakapo chaguliwa mwaka ujao.
Share






