Ripoti mpya kutoka shirika hilo ilipata ongezeko kubwa katika muda miaka 20 vyakuzama majini katika muda wa mwaka wa 2021 hadi 2022, wanaume walihusika zaidi katika takwimu za vifo hivyo.
Vilabu vya jamii vyaku okoa maisha navyo vimekuwa vikifanya juhudi zakulenga jamii mpya zawahamiaji wa Australia, kwa kutoa rasilimali katika lugha zao pamoja nakuandaa miradi inayo ambatana na tamaduni zao kutoa elimu kuhusu usalama ndani ya maji.
Kwa vifaa katika lugha yako kuhusu usalama ndani ya maji, na mwongozo wa jinsi yakuogelea, unaweza enda mtandaoni kwenye tovuti ya: drowningprevention.org.au kupata rasilimali mpya kutoka shirika la Royal Life Saving Australia.