Washindi wa mashindano yakitaifa ya lugha ya SBS kwa mwaka wa 2019, walitangazwa katika hafla iliyo sherehekea masomo ya lugha nchini Australia.
Shindano hilo linalo simamiwa na radio ya SBS, lilijumuisha washindani takriban elfu tatu miasita ambao wanajifunza lugha nchini Australia na washindani wana umri tofauti.
Mashindano ya SBS yakitaifa ya lugha ya 2019, yanaungwa mkono na shirika la Community Languages Australia na First Languages Australia, pamoja nakufadhiliwa na chuo cha taifa cha Australia.
Share





