Baadhi ya lugha hizo ni mpya nchini Australia, na idadi ya watu ndani ya jamii wanaozungumza lugha hiyo inaendelea kuongezeka.
Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilizungumza na mtayarishaji mkuu wa Idhaa ya Kirundi, Mireille Kayeye, kuhusu uzinduzi wa makala ya lugha hiyo mpya katika SBS Radio, pamoja na umuhimu wa hatua hiyo kwa jamii ya Warundi nchini Australia.





