Tathmini hiyo itatumia matokeo ya sensa ya mwaka huu, kuamua matoleo yake ya huduma za lugha kwa miaka mitano ijayo. Ila bila shaka, sawia na maswala katika siku hizi za janga, Uviko-19 itakuwa na sehemu yake pia.
Matokeo ya sensa yanaweza muliko uhaba wa uhamiaji kwa sababu ya mipaka kufungwa, hali ambayo itazua changamoto kwa tathmini ya huduma za lugha za SBS. Muda wa ushauriano ulianza tarehe Jumanne 5 Oktoba na, utadumu hadi 12 Novemba.
Kutazama nakufanya rasimu ya vigezo vya uteuzi, pamoja nakutoa maoni yako tembelea sbs.com.au/consultation.