Imetabiriwa kuwa chama cha Labor kita unda serikali ya wengi, wakati chama cha mseto cha upinzani L-N-P hakita timiza lengo laku ng’oa chama cha Labor madarakani hesabu za kura ya wiki jana zinapo karibia kukamilika.
Kwa sasa hesabu za kura zime kipa chama cha Labor viti 44 bungeni wakati inatarajiwa chama tawala kita salia na viti 48 bungeni hesabu za kura zitakapo kamilika. Wakati huo huo chama cha upinzani cha mseto cha L-N-P kime shinda viti 36 bungeni kwa sasa ila inatarajiwa chama hicho kita salia na viti 40 bungeni.
Hata hivyo hesabu kamili ya matokeo ya kura, inatarajiwa katika siku kadhaa zijazo nyingi yazo ziki amuliwa kupitia kura za upendeleo kwa kura zilizo pigwa mapema nakupitia posta.