Chama cha Labor kina elekea kupata ushindi wakihistoria katika eneo bunge la Bega jimboni NSW, wakati chama tawala cha Liberals kimepata matokeo mabaya sana dhidi yacho katika eneo bunge la kiongozi wa jimbo wa zamani Gladys Berejiklian la Willoughby.
Hesabu zinaendelea katika chaguzi za super Saturday jimboni NSW.
Ushindi wa chama cha Labor utakuwa wa kwanza katika eneo bunge la Bega, ambalo limekuwa chini ya uongozi wa chama cha Liberals tamngu eneo bunge hilo lilipo undwa 1988 na eneo bunge hilo lime ongozwa tangu mwaka wa 2003 na mbunge wake anaye staafu Andrew Constance.