Kwa mzazi, inaweza kuwa vigumu kujua chakufanya, mtoto wako akiwa mwathirika wa matendo ya unyanyasaji, au kama wao ndiwo wanafanya matendo hayo ya unyanyasaji.
Wataalam wamefanyia swala hili utafiti mpana, kujua chenye wazazi wanaweza fanya, kuwasaidia watoto wao kumaliza visa vya unyanyasaji. Hakikisha shule husika inajua kinacho endelea, na shirikiana nao. Kama mtoto wako amenyanyaswa au amenyanyasa, inaweza kuwa vizuri akizungumza na mshauri au shirika la Kids Helpline.
Kama mzazi, unaweza pata taarifa ya ziada kuhusu unyanyasaji kupitia mashirika ya Kids Helpline na Parentline, ambayo yanaweza toa huduma ya wakalimani.