Australia iki pata ushindi dhidi ya Peru, Denmark lazima ishindwe dhidi ya Ufaransa, kuwapa Socceroos fursa yaku endelea katika hatua ya mchujo.
Hata hivyo, kila kitu hakijawa sambamba kwa upande wa mechi hizo.
Hatma ya safari ya Australia na Denmark katika kombe la dunia, huenda ika amuliwa kupitia magoli.
Iwapo Australia itashinda mechi yake, na Denmark ishindwe dhidi ya Ufaransa, magoli kati ya timu hizo mbili yata tumiwa kuamua timu itakayo endelea katika hatu ya mchujo.
Australia ina ingia katika mechi hiyo, ikiwa imefunga magoli mawili, nakufungwa magoli matatu. Ilhali Denmark, imefunga magoli mawili nakufungwa moja.