Wadau wengi wa soka hawakuipa Australia, nafasi katika orodha ya timu zenye uwezo wakufuzu kutoka kundi lao la D la Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022.
Baada yakupewa funzo la soka katika mechi yao ya kwanza dhidi ya bingwa watetezi Ufaransa, wachezaji wa Australia walijua umuhimu wakupata matokeo chancha katika mechi yao dhidi ya Tunisia.

Mshambuliaji wa Australia Mitch Duke alifunga goli lakwanza na la pekee katika mechi hiyo, nakuipa Australia alama 3 mhimu ilizo hitaji.
Ushindi huo unamaana Australia kwa sasa ni timu ya pili ikiwa na alama 3 nyuma ya vinara wa kundi D Ufaransa ambao wana alama 6, wakifuatwa na Denmark na Tunisia ambao wana alama 1.

Hali hiyo inamaana kwamba Australia ikishinda au kutoka sare na Denmark katika mechi yao, Australia itafuzu katika nafasi yapili. Kwa upande mwingine, Denmark au Tunisia wakishinda mechi zao na Australia ifeli kushinda au kutoka sare basi, Socceroos watajiunga namashabiki wengine kutazama mechi zitakazo fuatwa za kombe la dunia kwenye runinga.






