Hatime ombi lao lilisikizwa na waandalizi wa michuano hiyo, ambao baada yaku wajumuisha wanawake michuano yao sasa ime ingia katika mwaka wa pili.
Timu ya wanawake kutoka jumuiya ya DR Congo, ni miongoni mwa timu za kwanza zilizo sajiliwa kushiriki katika michuano hiyo.
Nahodha wa timu hiyo Sofia pamoja na msaidizi wake Anna, walieleza SBS Swahili kilicho washawishi kushiriki katika timu na michuano hiyo, pamoja na mabadiliko ambayo wame ona katika maisha yao ya kila siku kiafya na kimwili tangu walipo jiunga na timu yao.