Timu ya soka ya Uhispania Sevilla FC itawasili nchini Tanzania leo

Andre Silva (C) celebrates a goal for Sevilla Source: AAP
Kwa mujibu wa msemaji wa Shirikisho la Soka la Tanzania Cliford Mario Ndimbo, wachezaji hao wanatarajiwa kuwasili jioni ya leo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam. Ndimbo alisema, timu hiyo ya La Liga ambayo ni maarufu duniani inadhaminiwa na SportsPesa, na licha ya kuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Simba SC pia ziara yao itahusisha matukio kadhaa ya kijamii na ya michezo ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa kliniki na mafunzo.
Share