Idhaa ya Kiswahili ya SBS ilizungumza na Rais wa Shirika la Kitwek la Magharibi Australia, Bw Steve Sitienei na aliweka wazi tofauti ya kampeni na ushawishi wa chama cha Labor na wapinzani wao wa chama cha mseto wa Liberal/Nationals katika jimbo la Magharibi Australia.
Bw Sitienei alitueleza pia matumaini ya jamii ya Magharibi Australia kwa serikali mpya ya chama cha Labor inayo unda serikali mpya, haswa wanachama wajamii ambao wanatafuta kazi.