Mamlaka wa afya jimboni Queensland wanajaribu kuelewa jinsi mwanafunzi wa sekondari aliye patwa na COVID-19 ana ungwa na wasafiri ndani ya karantini ya hoteli. Kesi mpya tisa ndani ya jamii za COVID-19, zimerekodiwa jimboni humo wakati wakaaji katika maeneo ya kusini mashariki wana endelea kuwa katika makatazo ya siku tatu. Kesi hizo tisa ni kubwa zaidi za maambukizi ya kila siku katika mwaka mmoja, na zote zime ungwa na mlipuko wa shule ya sekondari.
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimetoa wito leo Jumamosi kwa wafuasi wake kuandamana kutokana na kukamatwa kwa kiongozi wao Freeman Mbowe. Viongozi wa chama hicho wanasema wamewasilisha mashtaka mahakamani kupinga tuhuma za ugaidi zilizotajwa dhidi yake.
Madaktari 20 wa Congo wamekufa baada ya kupata maambukizi ya virusi vya Corona katika zaidi ya kesi 1,500 zilizorekodiwa tangu mwezi Machi mwaka 2020 katika jimbo la Kivu Kusini huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC).