Benki kuu ya Australia ime amua kuto ongeza kiwango cha hela taslim kwa 4.1% kwa mwezi wa pili mfululizo, ikidai kuwa viwango vya juu vya riba vinafanya kazi kupunguza mfumuko wa bei.
Uongozi mpya wa kijeshi nchini Niger Jumatatu umeishutumu Ufaransa kutaka ‘kuingilia kati kijeshi’ ili kumrejesha madarakani Rais aliyeng’atuliwa Mohammed Bazoum, huku mivutano ikiongezeka kati ya Niger na Ufaransa, iliyokuwa mtawala wa kikoloni kwa Niger, na majirani zake.
Rais wa Nigeria Jumatatu alitangaza hatua kadhaa za kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha, ikiwemo kutoa tani laki mbili za nafaka ya akiba baada ya ghala la chakula kuporwa kaskazini mashariki mwa nchi.
Mirengo ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja inaonekana kuchezeana mchezo wa paka na panya kuhusu mazungumzo ya maridhiano yanayotarajiwa kusuluhisha masuala tata nchini. Hilo ni licha ya Wakenya kuelekeza macho yao yote kwa vinara wa mirengo hiyo miwili Rais William Ruto na Raila Odinga mtawalia—kuhusu juhudi zao kutatua mzozo huo.
Matildas wajinusuru katika kombe la B la kombe la dunia, baada yaku adhibu Canada kwa magoli 4 kwa 0 nakufuzu kama vinara wa kundi hilo mbele ya Nigeria.