Mchumi maarufu nchini ameomba serikali icheleweshe awamu ya tatu ya makato ya kodi kwa ajili yakusaidia kukabiliana na mfumuko wa bei. Chris Richardson kutoka Rich Insight, ametabiri kuwa mwaka wa fedha wa 2024 utarejesha ziada ya dola bilioni 10, kupitia kodi za matumizi binafsi zitakazo toa mchango mkubwa zaidi.
Mtandao umekuwa sehemu salama ya ubunifu nakuungana kwa vijana wenye ulemavu, licha ya kundi hilo kuwa na uwezekano mara mbili zaidi yaku pitia uzoefu wa unyanyasaji mtandoani kila wiki. Takriban 70% ya walio shiriki katika kura ya maoni wamesema, wamepata ni rahisi kwao kuwa mtandaoni kuliko, wakati wako na watu ana kwa ana, wakati 45% yao wamesema kuzungumza na mtu anaye penda vitu kama wao ilikuwa moja ya vitu vizuri kuhusu intanet.
Uchunguzi wa bunge ume toa ripoti mbaya kwa mfumo wa wanao tafuta ajira nchini Australia, kuipata imefunga mashirika ya huduma kwa urasimu na ilifanya wanao tafuta kazi kutaweza kupata ajira. Tathmini hiyo yenye kurasa 650 kwa Workforce Australia** imetoa mapendekezo 75 yakufanya mageuzi nakujenga upya mfumo, ikiwa pamoja nakuhamisha ukaguzi wa kufuatilia kwa Centrelink badala ya mashirika mengine kutekeleza jukumu hilo.
Serikali ya Kenya imepania kuanzisha mfumo mpya wa afya utakaokuwa ukifadhiliwa na walipaushuru kwa kuwatoza asilimia 2.75 ya mapato yao kila mwezi, licha ya Mahakama Kuu kusimamisha mpango huo. Mswada wa Sheria zinazohusu Bima ya Afya ya Jamii (Jumla) 2023, endapo utaidhinishwa, utawezesha utekelezaji wa Sheria kuhusu Bima ya Afya ya Jamii 2023 iliyochapishwa wiki iliyopita kwa lengo la kuvunjilia mbali Bima ya Afya Nchini (NHIF) iliyodumu kwa miaka 57.
Ndege mbili za abiria zilizokuwa zimebeba watalii zimeanguka siku moja katika uwanja wa Kikoboga katika mbuga ya wanyama ya Tanzania lakini maafisa wamesema watu wote waliokuwemo ndani ya ndege hizo wamenusurika.
Kampuni ya Afrika Kusini itatengeneza kifaa maalum kinachoingizwa ukeni kwa wanawake ili kujikinga na maambukizi ya VVU, ambacho wataalam wa UKIMWI wanasema kitapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu. Baraza la Idadi ya Watu lilitangaza siku ya Alhamisi kuwa Kiara Health ya Johannesburg itaanza kutengeneza kifaa hicho kinachojulikana kama ‘silicone ring’ katika miaka michache ijayo, na kukadiria kuwa vifaa milioni moja vinaweza kutengenezwa kila mwaka.
Mwanamke nchini Uganda mwenye umri wa miaka 70 amejifungua watoto mapacha, daktari wake alisema siku ya Alhamisi, katika kile ambacho mama huyo alidai kuwa ni muujiza. Safina Namukwaya alielezea furaha yake ya kupata mapacha hao ambao walizaliwa siku ya Jumatano katika kituo cha matibabu katika mji mkuu wa Kampala, ambako alikuwa amepata matibabu ya uzazi.