Mweka hazina wa taifa Josh Frydenberg amesema kuwachagua wabunge huru, kutaweza sababisha vurugu na matatizo bungeni. Bw Frydenberg ame zindua kampeni yake ya uchaguzi, kwa ajili yakuhifadhi eneo bunge lake la Kooyong jimboni Victoria. Eneo bunge la Kooyong linajumuisha vitongoji vyakifahari kama Kew na Hawthorn, na eneo bunge hilo limekuwa moja ya eneo bunge salama la chama cha Liberal.
Mwili wa aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya, Mwai Kibaki, aliyeaga dunia Ijumaa wiki iliyopita, Jumamosi ulizikwa nyumbani kwake katika mji wa Othaya, jimbo la Nyeri, Kaskazini mwa mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Marehemu Kibaki alipewa heshima za kijeshi huku akipigiwa mizinga 19, kama njia ya kumuenzi amiri jeshi mkuu wa zamani. Kibaki aliongoza Kenya kati ya mwaka wa 2003 na 2013.
Wachunguzi wa tuhuma za rushwa zinazomkabili Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma wamesema kiongozi huyo wa zamani angefanya chochote ambacho familia ya Gupta mzaliwa wa India walitaka afanye kuanzia mwanzoni mwa muhula wake wa kwanza.