Taarifa ya Habari 1 Novemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya shirikisho na Victoria zimetangaza takriban dola milioni 880 za msaada kwa biashara, wakulima pamoja na mashirika yasiyo yafaida, ambayo yame achwa katika hali ngumu kufuatia mafuriko mabaya ya Victoria.


Mweka hazina wa shirikisho amesema sekta inaweza kabiliwa kwa wakati mgumu kukabiliana na ongezeko la bei za gesi na umeme. Jim Chalmers amedokeza aina fulani ya uingiliaji kati wa soko kupunguza bei, ambazo zinaweza ongezeka kwa hadi asilimia 50 katika miaka mbili ijayo.

Serikali ya New South Wales imesema haita toa huduma ya upendeleo kwa chama cha wafanyakazi wa reli, tram na basi. Waziri wa uhusiano wa waajiriwa Damien Tudehope alitoa madai hayo baada ya kuvunjika upya, kwa mashauriano na chama hicho kuhusu malipo na marekebisho kwa reli zamaeneo ya mji. Alex Claassens kutoka chama cha wafanyakazi wa reli, amesema maendele hayo mapya yanamaana kutakuwa hatua zaidi zasekta katika wiki mbili zijazo.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imemuita balozi wake wa Rwanda kurudi Kinshasa kwa mashauriano. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya DRC inasema “Kinshasa inatoa maelekezo kwa balozi balozi wake mpya nchini Rwanda, kuahirisha majukumu yake nchini Rwanda.” Uamuzi huo umetolewa saa chache baada ya DRC kumfukuza balozi wa Rwanda mjini Kinshasa. Rais wa Rwanda Paul Kagame ameandika ujumbe wa twiter kwamba amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres kuhusu uhasama unaoendelea kati ya Rwanda na DRC.

Idadi ya watu nchini Tanzania iliongezeka kwa zaidi ya asilimia 37 katika muongo mmoja hadi milioni 61.7, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Jumatatu, akionya changamoto zinazoletwa na ongezeko la idadi hiyo ya watu alipokuwa akizindua matokeo ya sensa ya kitaifa. Mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania, Dar es Salaam imesalia kuwa mkoa wenye wakazi wengi zaidi wenye takriban wakazi milioni 5.4, wakati visiwa vya Zanzibar vina watu wapatao milioni 1.9, ikiwa ni ongezeko la watu 600,000.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service