Taarifa ya Habari 1 Oktoba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Seneta wa chama cha Greens Jordan Steele-John amesema panastahili kuwa waziri washirikisho wa ulemavu, anaye stahili ongoza utekelezwaji wa mapendekezo kutoka tume yakifalme kwa ulemavu.


Mawakili wa utanzaji wa watoto wanaomba serikali ya shirikisho ipokee kwa haraka mapendekeo ya tume ya ushindani na wateja wa Australia [[ACCC]], yaliyo wekwa wazi katika ripoti ilyo chapishwa hii leo ((Oktoba mosi)). Ripoti hiyo imepata pia kuwa wazazi wenye mapato wastan ambao wana watoto wawili wanao pokea huduma ya malezi ya watoto, wanalipa takriban 16% ya mapato yao kwa malezi ya watoto, kiwango ambacho nicha juu zaidi miongoni mwa nchi wanachama wa O-E-C-D ambao kwa wastan hulipa 9% pekee.

Mji wa Sydney umerekodi mwanzo wa joto zaidi katika mwezi wa Oktoba, hali ambayo ime waweka mamlaka katika tahadhari ya juu, marufuki tisa kamili ya mioto ikiwa imetangazwa kote jimboni NSW. Ofisi ya utabiri wa hewa imesema nyuzi joto katika kituo cha Observatory Hill, zime pita nyuzi joto 35 hali ambayo imepita rekodi ya zamani ya nyuzi joto 33.1 iliyo rekodiwa katika miaka ya 1961 na 2009.

Wachimba migodi watatu walifariki na wengine 18 wanahofiwa kuzikwa baada ya shimo katika mgodi wa dhahabu usio rasmi nchini Zimbabwe kuporomoka, televisheni ya serikali imesema Jumamosi. Taifa hilo la Kusini mwa Afrika lina akiba kubwa ya madini ya platinamu, alimasi, dhahabu na shaba. Lakini kutokana na uchumi unaodorora, uchimbaji haramu wa madini umekithiri na mara nyingi hufanyika katika hali ya hatari.

Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Martin Fayulu Jumamosi alithibitisha kugombea urais kwenye uchaguzi wa tarehe 20 Disemba. Bw Fayulu ata kabiliana debeni na Rais Felix Tshisekedi, ambaye amekuwa tangu mwaka wa 2019 na anawania muhula wa pili.

Na katika michezo, wapinzani wanyang'anywa ushindi katika fainali za AFL na NRL nchini, wakati hatma ya timu ya raga ya taifa Wallabies ikiwa mikononi mwake itakapo ingia dimbani dhidi yawareno na vigogo wala vichapo katika ligi kuu ya soka ya Uingereza...


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service