Taarifa ya Habari 10 Aprili 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Baada ya wiki kadhaa za uvumi, hatimai waziri mkuu atangaza tarehe ya uchaguzi mkuu wa shirikisho, upinzani wasisitiza uko tayari kwa kampeni ndefu.


Wanafunzi katika ukanda wa northern rivers wa New South Wales, watarejea kusomea ndani ya madarasa 100 za muda, baada ya mapumziko ya shule wakati shule tisa katika kanda hilo yana endelea kufungwa kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko. Licha yakuwa mvua imepungua kote jimboni, hatari ya mvua inaendelea kuwa katika sehemu nyingi.

Marais Uhuru Kenyata wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, na Paul Kagame wa Rwanda Ijumaa wamezindua ramani iliyopanuliwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufuatia kuingizwa kwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuwa mwanachama mpya katika jumuiya hiyo. Rais wa DRC Felix Tchisekedi alitia saini mkataba wa kujiunga, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Nairobi iliyoandaliwa na Rais Kenyatta mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za EAC. Rais Kenyatta ambaye ni Mwenyekiti wa EAC alisema kujiunga kwa DRC kama mwanachama wa EAC kutaimarisha uchumi wa kikanda na ushindani barani huko na kote duniani. Wameongeza kusema kuwa kuingia kwa DRC katika EAC kutapanua biashara na ushirikiano wa kieneo.

Raia wa Ufaransa wameanza kupiga kura mapema leo Jumapili katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais unaotarajiwa kwenda duru ya pili kati ya rais anayemaliza muda wake na anaewania muhula wa pili Emmanuel Macron na kiongozi wa mrengo wa kulia Marine Le Pen ambayo itakuwa ngumu zaidi kuliko pambano lao la miaka mitano iliyopita. Kwa kulinganisha na wagombea wengine, Macron ametumia muda mdogo kufanya kampeni kutokana na vita vya Ukraine. Matokeo ya awali kadirio, ambayo kwa ujumla huwa sahihi, yatatangazwa mara tu baada ya uchaguzi kumalizika jioni ya leo.

 

 

 

 

 

 


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service