Serikali ya shirikisho inasita kurejesha malipo ya janga, hofu ikiongezeka kuhusu ongezeko la mlipuko wa UVIKO-19, utaendelea kudhuru zaidi wafanyakazi wa muda, ambao hawana haki yakupata likizo ya ugonjwa. Waziri ametangaza pia kuwa ustahiki wa dawa zinazo weza okoa maisha kwa coronavirus unapanuliwa. Wa Australia wenye miaka 70 na zaidi wanao patwa na virusi, wataweza pata dawa hizo kupitia mfumo wa faida yamadawa kuanzia kesho jumatatu, vile vile watu wenye miaka zaidi ya miaka 50 wenye hali za hatari mbili au zaidi kwa magonjwa sugu nawa Aboriginal au wanavisiwa wa Torres Strait wenye zaidi ya miaka 30 ambao wana sababu mbili au zaidi za hatari.
Kundi la watu limefanya mauaji ya wagonjwa tisa katika shambulio ndani ya kliniki mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasi ya kongo usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi ya Ijumaa, inalaumu wanamgambo wenye masimamo mkali. Wanamgambo hao wanaminika na jeshi kuwa ni ADF, kundi kutoka Uganda ambalo limekuwa likifanya harakati zake katika misitu ya Congo kwa miongo kadhaa.
Rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema kwamba haoni shida yoyote akiendelea kuongoza Rwanda kwa miaka mingine 20, na kuashiria kwamba atagombea muhula mwingine madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024. Kagame, mwenye umri wa miaka 64, ametawala Rwanda kwa zaidi ya miongo miwili. Amesema kwamba anajiandaa kwa muhula mwingine madarakani.