Taarifa ya Habari 10 Mei 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Kiongozi wa upinzani Anthony Albanese amethibitisha kuwa ataunga mkono, ongezeko la mshahara la zaidi ya 5.1% kuambatana na ongezeko la mfumuko wa bei.


Wafanyakazi wa huduma ya wazee wanao fanya mgomo kote nchini Australia, wamesema uamuzi wakususia kazi leo jumanne 10 mei, ulisababishwa na mazingira mabaya ya kazi ambayo wame sema yamekuwa mabaya kupindukia. Wafanyakazi kutoka makampuni tano makubwa Magharibi Australia na Queensland wamefanya mgomo, wakiomba ongezeko la wafanyakazi pamoja na ongezeko la mishahara.

Mwanaume mmoja ame okolewa kutoka maji ya mafuriko jimboni Queensland, mvua zisizo za kawaida zikinyesha katika eneo la kaskazini la jimbo hilo. Timu ya waokoaji wakasi majini kutoka huduma ya dharura na moto ya Queensland, ilimsaidia mwanaume mmoja nakumpeleka sehemu salama, baada ya mwanaume huyo kukwama katika maji yamafuriko katika eneo la Soldiers Hill, ambalo liko katika kitongoji cha Mount Isa, mida ya saa tano usiku wa jumatatu. Onyo la hali mbaya ya hewa ilitolewa kuanzia maeneo ya magharibi Townsville hadi Cloncurry, na kutoka maeneo ya Croydon kaskazini mwa jimbo hilo hadi maeneo y Blackall ambayo yako kusini mwa jimbo hilo.

Baraza Kuu la chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, siku ya Jumatano litatoa hukumu ya rufaa za wabunge 19 wanawake waliowafukuza uanachama kwa sababu ya kukiuka katiba na kanuni za chama hicho. Hatua hii ilichukuliwa baada ya wabunge hao kuchukua uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya chama hicho kuwapitisha. Chadema imesema Jumatatu Baraza Kuu la chama litasikiliza rufaa zilizowasilishwa na wabunge hao ambao wamefutwa uanachama.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service